Muhtasari na ufafanuzi wa moduli
Moduli hii yenye anwani ya Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili inakusudiwa kumjengea mwanafunzi misingi thabiti ya fasihi kwa jumla na fasihi ya Kiswahili. Hivyo basi, moduli hii inatalii kuanzia maana ya fasihi, asili ya fasihi, dhima za fasihi, historia ya fasihi ya Kiswahili, uanishaji wa tanzu mbalimbali za fasihi ya Kiswahili na uhakiki wa fasihi ya Kiswahili na maswala mengine kuhusu fasihi na tanzu zake. Hivyo mwanafunzi anajengewa misingi thabiti juu ya nadharia ya fasihi na misingi ya uhakiki na uanishaji wa fasihi ya Kiswahili. Mwishowe, ni fasihi kama nyenzo ya utekelezaji wa mtaala unaoegemea katika uwezo.
- Lecturer: RUHUMULIZA GASPARD
- Lecturer: STANISLAS MUNYENGABIRE